Agano Jipya

Utukufu wa Agano Jipya unayagusa maisha ya kila mtu aliyezaliwa mara ya pili. Yesu Kristo alipokufa na kufufuka kutoka kwa wafu, Sheria iliondolewa na tukafanyika watu huru, tunaoishi chini ya neema! Hatufungwi tena na kanuni na sheria kwa kuwa tumeingia katika uhusiano mpya kabisa na Mungu, tukiwezeshwa kuingia moja kwa moja mbele zake na kumtumikia kutoka ndani ya mioyo yetu.

Huduma Tano

Inasikitisha kuona Wakristo wengi wanaokiri uwepo wa Huduma Tano wakishindwa kuuona umuhimu wake au hata kuelewa namna hizi huduma zinavyopaswa kulihudumia Kanisa. Wengine wanapatwa na wasiwasi juu ya athari zake kwa huduma zao binafsi na wanaamua kuzifumbia macho. Lakini, pasipo kujali Imani ya mtu mmoja mmoja, ni wazi hakuna Mkristo mkweli atakayesema ya kwamba vipawa ambavyo Yesu anatoa kwa wanadamu katika kuliongoza na kuliandaa Kanisa lake vilikuwa ni kwa ajili ya Kanisa la Mwanzo tu. Kila kitu kilichoandikwa kwenye Agano Jipya kuhusu utendaji wa hizi huduma tofauti katika kulijenga Kanisa litahusika maadamu Kanisa lidumupo duniani. Roho yule yule aliyekuwepo wakati Kanisa linaanza, bado yuko kazini hata leo. Yesu hajabadilika.

Kanisa Linahitaji Kujua

Hebu sote tukubaliane ya kwamba kwa namna moja au nyingine Kanisa limeliacha fundisho la uzima, na matokeo yake yanaonekana katika maisha ya watu wa Mungu. Umefika wakati tuyazungumzie mambo fulani ya msingi waziwazi, ili Wakristo watambue ya kwamba Bwana ana mambo mazuri zaidi kwa ajili yao, makusudi watembee katika uhuru na katika ushindi!